'Bado kuna hali ya ati ati kuhusu hatma ya Pogba uwanjani Old Traford

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba alisema mwamba bado kuna hali ya swintofahamu kuhusu hatma yake katika timu ya Manchester United licha ya ushindi wao mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili katika mchuano wa kwanza wa ligi ya primia.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa ufaransa alitaka sana kuondoka Man United wakati wa likizo baada ya kukamilika kwa msimu wa ligi huku akihusishwa na uhamisho kujiunga na Real Madrid au Juventus.

Meneja Ole Gunner Solskjaer alipongeza mchango wa Pogba baada ya kuandaa bao la tatu na la nne dhidi ya Chelsea, lakini kiungo huyo alisema "ni muda tu utakao amua" ikiwa atasalia nchini Uingereza.

“Mimi huhisi vyema nikicheza soka. Nafanya vitu navyopenda, tena ni kazi. Najituma kila wakati nikienda uwanjani,” Pogba aliambia kituo cha radio cha Ufaransa RMC.

“Nafahamu kwamba kuna mambo ambayo yamesemwa. Ni muda tu utakaoamua. Bado patakuwepo alama ya duku duku.

“Niko katika timu ya Manchester. Nafurahia muda na wachezaji wenzangu. Kila wakati nataka kushinda mechi nami hufanya kadri ya uwezo wangu uwanjani.”

Kipindi cha uhamishi wa wachezaji kilifika tamati Alhamisi, siku moja kabla ya kuanza kwa msimu mpya, lakini vilabu nchini uingereza bado vinaruhusiwa kuuza wachezaji hadi kukamilika kwa kipindi cha ihamisho barani Eropa Septemba tarehe mbili.

TAARIFA IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO