Penzi la peni mbili larejelewa,Mustapha na Noti flow kitu moja

NOTI FLOW
NOTI FLOW

NA NICKSON TOSI

Baada ya miezi ya pantashuka na udanganyifu katika uhusiano wa Colonel Mustapha na Natalie Florence almaarufu kama Noti kuenea mitandaoni,sasa wawili hao wamerudiana pamoja.

Kwa siku mbili mfululizo,Mustapha na Noti wamekuwa wakitundika picha zao wawili katika mitandao ya kijamii wakielezea wafwasi wao kuwa wamerudiana.

Colonel Mustapha aliandika hivi,

“Ball imerudi home ground,” shared Colonel Mustapha.

Siku ya wapendanao tarehe 14 febrauri mwaka huu,Noti Flow alipiga picha na Mustapha wakiwa karibu na kidimbwi cha kuogelea kisha kuwatakia wapenzi wote siku njema ya Valentino.

Kulingana na Mustapha waliafikia kuweka kando tofauti zao na kuamua kurejelea uhusiano wao ambao aliutaja kama uliokuwa wa manufaa kwake.

Aliandika hivi Mustapha .

“Today was a good day. Happy Valentines Queen 🌹❤️,” wrote Mustafa.

Akamjibu Noti Flow “Valentines”

Mwisho wa mwaka jana ,Noti Flow alichangia maoni ya msanii Trap King Chrome kuwa Mustapha ni shoga kutokana na mzozo wao ulikuwa umeibuka baina ya wapenzi hao.

Aliandika hivi Noti Flow,

“You guys @trapkingcrome was right. Mustafa is gay and he lives with his boyfriend in Utawala! Confirmed.wow Fake ass Muslim,” alisema Noti Flow.

 

Madai ambayo Mustapha alikana .

“I live in Utawala, na ile nyumba inaruhusiwa kuingia mamangu mzazi na inaruhusiwa kuingia mtu yeyote kuingia kwa ile nyumba na tunasali sana. I think yeye alichanganikiwa alipotukana muslim cz alitukana muslim cz akipiga simu anaskia yale maadili pale ni ya kiislamu," stated Mustapha.