Penzi la sumu? Tazama waliopendana licha ya pingamizi kutoka kwa jamii-Kuanzia kwa Tecra Muigai hadi kwa Wambui Otieno na Princess Diana

Mapenzi hayana mipaka  na wengi wamejipata katika matatizo ya kupenda mtu ambaye familia au jamii haimtaki lakini wakaendelea kufanya mambo yao wanavyotaka. Wengine walipendana licha  ya kuwepo pengo kubwa la umri kati yao na ulimwengu ukashangaa jinsi uhusiano wao ungedumu.  Tofauti ya rangi  pia  ilizua mihemko wakati  wapendanao kama vile Prince Harry na Meghan Markle walipotangaza kwamba wanataka kufunga ndoa.

 Tecra Muigai na Lali Omar

Kisa cha Tecra  Muigai na Lali Omar sio cha kwanza kama cha Bonnie la Clyde kwani hapo awali pia kulishuhudia visa vya watu wawili waliokaidi matakwa ya ulimwengu mzima kupendana licha ya kuwepo pingamizi. Marehemu Tecra Muigai yuadaiwa alikuwa ameishi maisha yake kivyake na kwamba familia yake haikumtaka  mpenzi wake Omar Lali.  Yadaiwa familia  yake ilimlaumu Lali kwa mtindo wa maisha ya binti yao na hata hali iliyosababisha kifo chake ipo chini ya uchunguzi kwani alikumbana na mauti yake akiwa na Lali huko Lamu.  Pindi picha za Lali zilipowekwa mitandaoni, ungetazama maoni ya wakenya ili ufahamu jinsi wengi walivyokuwa na maoni mengi kuhusu uhusiano wa wapenzi hao .

 Wambui Otieno na  Peter Mbugua

Mapenzi yao yaliteka  ndimi za wengi miaka 17 iliyopita wakati Wambui Otieno aliyekuwa na umri wa miaka 67 wakati huo alipoamua kudunga ndoa na  Peter Mbugua aliyekuwa na umri wa miaka 29. Wengi walikuwa na mengi ya kusema kuhusu mapenzi yao na baadaye  ndoa yao. Watu walishangaa mwanamke mwenye umri kama wa Wambui alitaka kujinufaisha vipi kwa kujihusisha katika mapenzi na kijana wa umri wa miaka 29. Isitoshe, Mbugua alikuwa na mke wa rika  lake ambaye  alimtelekeza ili kuwa an Wambui. Lakini mapenzi yao  hayakudumu kwani pindi Wambui alipoaga dunia mwaka wa 2011, familia yake ilimfurusha Mbugua kutoka boma lao na papo hapo penzi lao lilizima.

  Princess Diana na  Dodi  Fayed

Princess Diana  na Dodi Fayed waligonga vichwa vya habari  Agosti mwaka wa 1997 baada ya kuaga dunia katika ajali mbaya jijini Paris.Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi  kwa miezi miwili  na kabla ya kufichuliwa kwa uhusiano wao, ndoa ya Diana  kwa Prince Charles ilikuwa imevurugika kabisa. Mapenzi ya Diana na  Fayed, raia wa  Misri yaliwafanya wengi kuzungumza kwani wakati huo kila mtu alisema uhusiano huo haungedumu. Diana wakati mmoja alikiri kwamba  uhusiano wake na Dodi ulikuwa wa kupitisha muda tu kwani baada ya kupitia ndoa yenye matatizo mengi na Prince Charles hakuna aliyemtarajia kujitosa katika ndoa nyingine kwa haraka kama na Dodi .

Diana alikuwa amehofishwa  sana na athari ya uhusiano wake na Dodi kwa watoto wake wawili na pia kile ambacho kingesemwa kumhusu na familia ya kifalme ya Uingereza .

 Emmanuel Macron na

Rais wa Ufaransa Emmanuel  Macron na mkewe wana mapenzi ambayo pia yaliuteka ulimwengu kwa ajili ya tofauti kubwa ya umri wao. Brigitte akiwa na umri wa miaka 40 alikutana na Emmanuel aliyekuwa na umri wa miaka 15  katika shule ya msingi ya La Providence mwak wa  1993. Brigitte alikuwa mwalimu wa Macron na kama wanavyosema ajuaye kesho ni Mola, baadaye walikutana tena na  kufunga ndoa. Brigitte alitalakiana na  mume wake Auzière mwak wa 2006 na kufunga  ndoa na Macron  Oktoba mwaka wa 2007. Rais Macron alipokuwa  mwanafunzi alikuwa katika darasa moja na binti  yake Brigitte, Laurence.

Prince Harry  na Meghan Markle

Prince  Harry na muigizaji Meghan Markle  walipotangaza mpango wao kufunga ndoa, wengi kote duniani walishangaa endapo uhusiano wao ungeungwa mkono na familia ya kifalme Uingereza. Markle alikuwa anamzidi Harry kwa umri na isitoshe mamake alikuwa mweusi. Hakuna aliyejua iwapo  familia ya kifalme ilikuwa tayari kumkaribisha mtu mweusi katika  ufalme wake. Hata hivyo, miaka miwili baada ya kuoana, Harry na Meghan waliushangaza ulimwengu wa kutangaza kwamba wanataka kuondoka kutoka familia kuu ya kifalme. Malkia Elizabeth inaripotiwa alijaribu kuwashawishi wasiondoke lakini wawili hao walikuwa wameshafanya uamuzi wa kuanza upya maisha yao.