'Pesa chafu' katika ununuzi wa ngano Narok, CBK yatilia shaka

CURPIC
CURPIC
Benki Kuu ya Kenya inatilia shaka kisa na ambapo idadi ya wanunuzi wa ngano wameongezeka kaunti ya Narok.

Kuna uwezo mkubwa walaghai wanatumia noti mzee za elfu kuwarubuni wakulima katika kaunti hiyo.

Haya yanafanyika huku Gavana wa CBK akionya kuwa Tarehe ya kubadilisha noti hizo haitaaihirishwa.

Soma hadithi nyingine:

Wakenya ambao hawatakuwa noti zao watapoteza pakubwa.

Dkt. Njoroge amesema kuwa wafungwa katika jela wataruhusiwa kubadilisha noti hizo kwa usaidizi wa mahakama.

Ikumbukwe kuwa kuna idadi kubwa ya noti mzee za elfu moja zilizoshikwa mateka kama ushahidi katika mahakama nchini.

Gavana wa CBK anasema kuwa iwapo mahakama hazitabadilisha hela hizo basi zitapoteza thamani.

Soma hadithi nyingine:

Serikali alizamia mageuzi ya noti hizi ili kupambana na utengenezaji wa noti feki.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Patrick Njoroge amewaomba wakenya wawakumbushe wakongwe katika jamii wawajibike katika zoezi hilo.

“Wamama ,nyanya wetu wanapenda kuwekeza sana. Kuna uwezekano wana noti hizi mzee nyumbani.” Njoroge alichapisha ujumbe kwa Twitter.

Noti hizi zikifikishwa katika tawi za Benki Kuu ya Kenya, zitasafirishwa katika lori hadi kwenye makao makuu.

Soma hadithi nyingine:

Maafisa wakubwa watapanga siku na ambayo watakusanya noti zote.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, noti hizi mzee zitakatwakatwa katika vipande vidogo na baadaye kuchomwa hadi ziwe jivu katika eneo la Kariobangi jijini Nairobi.