Pesa husumbua watu! Mwanamme wa India anunua maski ya dhahabu kukabiliana na coronavirus

pjimage (1) (1)
pjimage (1) (1)
  Mwanamme mmoja nchini  India ametumia shilingi laki nne kununua  maski ya dhahabu ili kujikinga dhidi ya virusi vya corona .

Maski hiyo ina uzito wa gramu 60  na iliwachukua wasanifu wa  bidhaa  siku nane kumtengezea mfanyibiashara  Shankar Kurhade, maski hiyo spesheli .

" Ni nyembamba  na ina mashimo madogo amdogo yanayokuwezesha kupumua  ,sina uhakika iwapo itanilinda dhidi ya virusi lakini nachukua tahadhari nyingine’  amesema  Shankar

Anapoondoka kwake kwa shughuli za kila siku  mfanyibiashara huyo hupenda kujistiri kwa dhahabu ikiwemo mshipi wake , shanga  na mkufu  vyote vyenye uzito wa takriban kilo moja .

Kurhade --  amesema alipata  wazo la kutengezwa maski ya dhahabu baada ya kuona katika vyombo vya habari mwanamme mmja akivalia iliyotenegezwa kwa fedha .

" Watu wanataka  nipige nao selfie’ amesema

India imefanya uvaaji wa maski kuwa jambo la lazima  katika maeneo ya umma  baada ya visa zaidi ya laki sita  kuthibitishwa na  watu 18,600 kuaga dunia .