Pesa ni sabuni ya mwanamke: Mwanamme aachwa hoi na mkewe aliyetoroka na bosi tajiri

man
man
Umaskini una gharama. Ingawaje pesa sio kila kitu, pesa wakati  mwingine ni muhimu  wakati wa kushindania  penzi la mwanamke anayethamini pesa kuliko penzi halisi .

Hebu firikia unachoweza kufanya iwapo mkeo angetoroka  na bosi wake kwa sababu bosi ana pesa kukuliko. Ndio makubwa yaliyompata Petro  Kibuga baada ya mke wake wa miaka minane kuacha ndoa yao ili kuanza maisha upya na bosi wake na kuzidisha  uchungu katika kidonda cha Petro akamchukua pia mtoto wao mvulana aliyekuwa na umri wa miaka 5.

‘Angeniacha kwa sababu nyingine basi ningekubali, lakini kwa sababu ya pesa? Nilimdharau zaidi.’ Anasema Petro

Hadi leo  Petro hajaamini kwamba  Isabel alitupa nje kila kitu walichojenga na kupanga katika maisha yao ili kumuendea mwanamme aliyekuwa na pesa ambaye pia alikuwa na familia nyingine na sasa  Isabel ni mke wa pili. Bosi wa mke wake alikuwa maneja mkuu wa  kampuni moja ya bima nchini. Mke wake Isabel alikuwa amepewa kazi katika kampuni hiyo kama msimamizi wa mauzo kumbe kazi hiyo ilimfanya kukaribiana sana na bosi hadi wakaanza kushiriki mapenzi. Isabel yaonekana alivutiwa na pesa na magari makubwa makubwa ambayo bosi huyo alikuwa akija nayo kazini lakini hakujua kwamba jamaa yule ni kama fisi. Alikuwa akitafuna kila kinachopita machoni pake na wakati ule Isabel ndiye aliyekuwa kondoo mgeni ambaye ameleta mnofu machoni  pake.

‘Sijui mbona baadhi ya wanawake hupenda pesa zaidi ya waume zao katika ndoa.’ Anashangaa Petro

Muda  mfupi baadaye, Petro anasema mke wake aliuza gari lao dogo na kuja nyumbani na bonge  la gari zito la Mercedes Benz. Alipatwa na mshangao mume wa mtu kujua kwamba mke wake kaja na Benz! Ametoa wapi pesa? Hilo ndilo swali ambalo alitaka jibu  lakini hakupewa. Isabel baadaye baada ya kulazimishwa kusema alikotoa pesa alikiri wazi kwamba baada ya kuuza gari lile dogo, bosi wake kamuongezea pesa ili anunue lile gari jipya.

‘Uchungu wa  mke wangu kutoroka ulizidishwa na yeye kwenda na mtoto wangu’  anasema Petro

Malumbano kati yao yalizidi na muda sio mrefu, Isabel aliamua kuchukua kila kilicho chake pamoja na mtoto wao na kuhamia katika nyumba ya kifahari ambayo alikodoishiwa na Yule bosi. Maskini Petro aliachwa mtaa wa  akina yakhe Kawangware huku Isabel akitesa mtaa mpya wa kifahari wa Karen. Walipooana, mwanamke hakuwa hata na  ujuzi wa kuvalia ‘high heels’ kwa sababu ya ‘ushamba’ lakini duh! Kaposti picha zake mtandaoni akiwa katika viatu ambavyo urefu wake  ungekushangaza wewe.

Akifiriki labda ulikuwa uhusiano wa muda tu kati ya mke wake na bosi wake na baadaye atapatwa na fahamu na arejee nyumbani. Basi Petro alikuwa akichelewa sana kupatwa na mshtuko. Mke wake alikuwa na mimba ya bosi wake! Maneno yalimuisha na matumaini yakamhepa. Hakujua kwamba kukosa pesa au cheo vile ni jambo ambalo lingeivunja ndoa yake. Tamaa kweli haina mipaka na usaliti hauna ustaarabu. Yamkini asiyekujali kamwe hana huruma kwako na  Petro kwa sasa anaendelea na jitihada za kuyasahau mahangaiko ya miaka miwili iliyopita baada ya kuanza uhusiano mpya na mwanamke mwingine kwa lengo la kufunga ndoa nyingine. Mnyonge hana haki jamani!