Pesa Otass: Hassan Joho na Junet Mohamed watumia ndege ya kibinafsi kwenda kumtembelea Raila Dubai

Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho na mbunge wa Suna mashariki Junet Mohamed Jumanne walisafiri kwenda nchini Dubai ili kumtembelea kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Wawili hao waliposti picha za safari yao huku, picha nyingi zikionyesha ndege ya kibinafsi waliotumia kusafiri kwenda nchini humo.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter, kwa utani, Junet alimuuliza wakili Ahmednasir Abdullahi asiwaonee wivu kwa ajili ya safari yao.

"Off to Dubai with @HassanAliJoho to see Baba. SC @ahmednasirlaw don’t feel bad. He is BABA!" Junet Aliandika.

Usafiri wa ndege wakati huu umekuwa kwa matajiri baada ya ndege kutoka nje kukomeshwa kuingia nchini kwa ajili ya virusi vya corona.

Gharaama ya kutumia ndege ya kibinafsi ni ya juu huku kwa risali moja ndege ikikombolewa kwa shillingi 100,000 kwa saa moja na hata nyingine ukombolewa kwa shillingi 800,000 kama ile wanasiasa hao wawili walikuwa wanatumia.

Kukomboa ndege kutoka hapa hadi nchini Dubai ni takribani masaa manne ili kutua nchini humo, Jumatatu wiki hii rais, Uhuru Kenyatta alifungua mipaka na kusema kuwa ndege za kimataifa zitaanza ktua nchini mnamo tarehe 1 Agosti mwaka huu.

Hizi hapa baadhi ya picha zao;