PIC yaonya kuhusu ufujaji mkubwa katika hazina ya vijana

Picha: Twitter

Kamati ya bunge inayochunguza madai ya kupotea kwa shilingi milioni 400 katika hazina ya ustawi wa vijana imeonya kuwepo kwa sakata nyingine ya ufujaji mkubwa wa pesa za umma.

Huku sakata hiyo ikifichuliwa, majina ya aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru na katibu wake wa kudumu Peter Mangiti yametajwa tena katika sakta hiyo. Wabunge wa kamati hiyo ya uwekezaji wa umma walitaka kujua mbona mwenyekiti wa bodi ya hazina hiyo Bruce Odhiambo alimfuta kazi maneja wa kifedha Benedict Atavachi kisha akawaandikia barua Mangiti na Waiguru kuwaarifu kuhusu hatua hiyo.