+ Picha ) Alichokibeba Paul Manyasi katika 'safari' ya ndege, jina lake la msimbo

Paul Manyasi alikuwa amejihami na vitu kama chupa ya soda, maji ya kukata kiu na mfuko ambao aliubeba katika 'safari' yake ya kuzuru Uingereza.

Mwili wa kijana huyu wa Kakamega ulianguka katika shamba la maua ndege ilipochomoa magurudumu kutua Juni 30 nchini Uingereza.

Marafiki wamesema kuwa jina la utani la Paul Manyasi lilikuwa MCA (Member of County Assembly).

Je, huenda ikawa Paul Manyasi alikuwa na nia ya kuwa mwakilishi wodi?

Tukio la jana la aliyekisiwa kuwa babake kijana huyu Mzee Isaac Munyasi kumkataa limefanya swala hili kuwa ngumu zaidi.

Shirika la habari la Sky News linachunguza kwa makini kubaini wazazi wake Paul.

'Baba' huyu alisema kuwa huyo sio mtoto wake.

Anahisi kuwa mwanawe bado yupo hai.

Alisema kuwa mwanawe anaitwa Cedric Shivonje na atazamia jiji la Nairobi kumtafuta.

Iwapo atamkosa mwanawe basi itabidi DNA au vinasaba kufanyika ili kubaini ukweli.

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ Juni 30 kiliwatia wengi hofu kubwa.

 Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa JKIA taarifa na ambazo shirika hili limekataa.