+ Picha ) Familia ya Paul Manyasi yamgeuka, yasema kijana wao ni Cedric

Familia ya kijana aliyeanguka kutoka kwa ndege ya KQ imegeuka ghafla na kumkataa.

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ kiliwatia wengi hofu kubwa.

Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa KAA.

Familia inasema kuwa mwana wao ni Cedric Shiunja wala sio Paul Manyasi.

Aidha picha zilizotolewa na Sky News zinakinzana na zilizopo katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Familia inaongezea kuwa hawajui mwanao alipo na wamekataa taarifa za kuhusishwa na mwili wake Paul.

Shirika la habari la Sky News lilihoji kuwa lilipata nafasi ya kusema naye 'baba' wa kijana huyu.

"Niligutushwa sana na habari kuwa Paul ni mwanangu licha ya kuonyesha ripota huyo picha tofauti ya mwanangu na kuwaambia kuwa picha walionionyesha sio ya mwanangu...nitawashtaki," alisema baba huyo.

Mamlaka ya ndege nchini imekana taarifa kuwa Paul alikuwa mfanyakazi wao.

Mwili wa kijana huyu ulianguka kwa kishindo huku shimo kubwa likichimbika katika shamba la maua kusini mwa mji wa London wakati magurudumu ya ndege hilo yalichomoka ili itue.

Baba huyu ameisimulia KTN kuwa hajui aliko kijana wake Cedric Shivanje ili anahisi kuwa ameshikwa na maafisa wa polisi.

"Nilipata taarifa kutoka kwa kijana fulani ambaye anatoka Kakamega na anaishi Nairobi, aliniambia wiki iliyopita kuwa mwanangu alikamatwa na anazuiliwa...."  Alisema mzee huyu.