(+ Picha) Hali halisi, Usahihishaji wa KCSE wasitishwa kituo cha Machakos

Screenshot_from_2019_12_03_11_30_21__1575361849_53820
Screenshot_from_2019_12_03_11_30_21__1575361849_53820

Usahihishaji wa karatasi za mtihani wa KCSE katika kituo cha shule ya upili Machakos umesitishwa kwa muda kufuatia kile kinachotajwa kama mazingira mabaya kuhusu malazi yao.

Zoezi hili linaloendelea kwa sasa linahofiwa kutatizika iwapo swala hilo halitatuliwa.

Idadi ya walimu 700 wameagizwa kusitisha zoezi la kusahihisha.

Walimu hawa walikuwa wamefanya maandamano kwa siku mbili hapo awali wakilalama mazingira mabaya ya utendakazi.

Katibu wa muungano wa kutetea haki za walimu katika mwavuli wa chama cha KUPPET Akello Misori amedhibitisha kuwa walimu hao wameondoka katika kituo hicho baada ya juhudi za kuwasilisha lalama zao kugonga mwamba bila suluhu yoyote.