(+Picha )Harmonize aifunika tatoo aliyochora ya Diamond kwa michoro

Screenshot_from_2019_12_10_10_27_02__1575962853_14427
Screenshot_from_2019_12_10_10_27_02__1575962853_14427
Ni wazi na bayana kuwa staa wa muziki Harmonize hataki kabisa kuonekana na tatoo aliyojichora ya bosi wake Diamond Platnumz.

Tatoo hii aliichora kipindi na ambapo alikuwa chini ya lebo ya Wasafi.

Alikuwa ameichora kuonyesha ni kwa kiasi gani anavyothamini nafasi aliyopewa ya kujulikana kuwa ana kipaji duniani.

Diamond alikuwa mtu wa kwanza kugundua kipaji cha Harmonize na akawekeza katika kipaji chake katika hali ya kumsaidia atoke kimuziki.

Hatimaye Harmonize aliitema lebo hii na kuanzisha yake ya Konde Gang.

Kwa kile kinachoonekana kama kujisahau na kuingiwa na ustaa mwingi, Harmonize amefunika tatoo hiyo na michoro mingine.

Ushikaji umepotea kati ya mastaa hawa wawili.

Katika fiesta iliyofanyika uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam, Konde Boy alikosa kumtaja Diamond katika phrase aliyomtaja ya ngoma ya Uno.