PICHA: Hawa ndio wanasiasa walio na mitindo ya kuvutia zaidi nchini

Mbali na siasa tu, kuna wanasiasa ambao hujivisha vizuri sana na mara kwa mara huwakata watu shingo wanapopita.

Gavana wa Mombasa, bwana Hassan Joho na seneta wa Nairobi bwana Johnson Sakaja ni baadhi tu ya wanasiasa ambao mtindo wao wa kuvalia umegonga ndipo.

1.Najib Balala

Waziri wa Utalii bwana Najib Balala huwa anavalia vizuri sana iwe ana mkutano au yuko kwenye matembezi ya kuijiburudisha.

kwa mfano, tazama picha ya waziri huyu anavyopendeza.

2.Hassan Joho

Mheshimiwa Joho, ajulikanaye kama Sultan, ni gavana wa Mombasa ambaye amejulikana kwa kuwa na ndevu zilizo nyolewa kwa ustadi.

Zaidi ya hayo, Joho huongeza mapambo kama saa na miwani ambayo humfanya ang'ae.

Esther Passaris

Esther Passaris ni mfanyi biashara, na mwanasiasa wa humu kenya.

Binti huyu ambaye ni kiongozi wa wanawake mjini Nairobi ana mtindo mzuri sana wa kuvaa.

Zaidi ya hayo, Passaris akiwa amesonga nywele zake ama akiwa na nywele yake yenyewe, huwa anapendeza kupita kiasi.

Mike Sonko

Mike Sonko ni gavana wa Nairobi na tangu apate cheo cha bunge, alibadilisha mtindo wake wa kuvaa na ni bayana kuwa, mtindo huu wa kuvaa umemfaa sana.

Peter Kenneth

Bwana Peter Kenneth naye ni mwanasiasa ambaye hakuna siku amewaaibisha wakenya kwani suti na saa zake huwa zinapendeza kila kuchao.

Licha ya mavazi yake, tabasamu la mheshimiwa huyu huongeza uzuri wake.

Sakaja Johnson

Seneta wa Nairobi bwana Sakaja naye hajaachwa nyuma kwani pia yeye huvaa vizuri sana iwe amevaa suti au nguo za kustarehe tu.

Gideon Moi

Mwanasiasa huyu ambaye ni gavana wa mtaa wa Baringo ana mtindo wa kuvaa ambao hufanani na mwanasiasa yeyote.

Mara kwa mara, Gideon Moi huvaa sweta nzuri ndani ya suti aayovaaa.

James Orengo

James Orengo ni mwanasheria ambaye huvaa suti ambazo hung'aa sana na mara kwa mara yeye huvaa rangi ya samawati ambayo hupendeza sana kila wakati.

Amina Mohamed 

Binti huyu ni waziri wa michezo na mtindo wake wa kuvaa huwapendeza wengi sana kwani yeye huvaa  nguo za heshima sana.

Amina Mohamed huvaa mtandio kila mara na mitandio hii ndiyo kumtofautisha na mawaziri wegine.

Charity Ngilu

Mwanasiasa wetu Charity Ngilu ni binti mwengine pia ambaye huvaa vitenge mara kwa mara na huwa anapendezwa sana nguo zake.