(+Picha) Jared Okello amtembelea Akothee hospitalini, amtakia afueni

Msanii wa kizazi kipya Akothee amefurahi sana kwa kutembelewa na ndugu za mume wa kwanza hospitalini.

Jared alikuwa mpenzi wa kwanza wa Akothee.picha-jared-okello-amtembelea-akothee-hospitalini-amtakia-afuenipicha-jared-okello-amtembelea-akothee-hospitalini-amtakia-afuenipicha-jared-okello-amtembelea-akothee-hospitalini-amtakia-afueni

Staa huyu wa kike alilazwa hospitalini baada ya kuzirai na kuanguka stejini akitumbuiza katika Luo Festival iliyoandaliwa mji wa Kisumu muda mchache nyuma.

Wengi wa mashabiki walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa burudani wikendi katika fiesta waliposhuhudia kisa hiki.

Wengi walimtumia jumbe za kusema pole na kumtakia afueni ya haraka.

https://www.instagram.com/p/B53JeSZHNrs/

Mumewe Jared Okello alifika ili kumjulia hali na kumtakia uponyaji wa haraka.

 "Kutana na familia yangu. Jakwath Jared Okello na ndugu zake walinitembelea. Heshimu baba Vesha...' Alichapisha Akothee.

"Hakuna kinachoweza kufunika mambo ya kale. Ninaomba nawe pia uweze kuwa na amani na ndugu  zako kwa manufaa ya wanao... "alisema Akothee.

Akothee aliwataka watu ambao wana mizozo katika ndoa au ata familia kuisuluhisha ili wakuwe sawa katika maisha.

"Naomba tuwe na amani kati ya wanandoa kwa sababu ya watoto wetu , dunia ni tambara mbovu..."Alisema Akothee.