(+Picha) Jumba freshi la Njugush na mkewe Celestine, baraka za Mungu

njugush
njugush
Mcheshi Njugush na mkewe Celestine ni kati ya watu maarufu ambao wameanza maisha katika hali ya kinyonge na uchochole mwingi.

Njugush ni mfano wa kuigwa baada ya kuwa na mafanikio mengi yanaoonekana kutokana na bidii na mchango mkubwa katika tasnia ya ucheshi nchini.

 Jumba lao ambalo wamemaliza kulijenga pia ni ishara kuwa Njugush anaangukia dili freshi na ambazo zinalipa kima kikubwa cha hela.

Haya yanajiri huku mcheshi huyu akihakikisha penzi lake kwa Celestine kuwa litazidi kuwa imara.

Katika mtandao maridhawa wa Insta, Njugush aliposti ujumbe mrefu kuonyesha uaminifu wake kwa mpenzi wake.

"Happy 3rd Celestine, nikapata nafasi nyingine ya kuoa ningechangua ile kuku tulikula pale high table. Its what I was thinking about in the last pic ..."