KQ 1

[Picha ] KQ yafanya ziara ya kwanza London baada ya zafari za kimataifa kuanza

Shirika la safari za ndege nchini Kenya Airways  limerejea usafiri wa kwenda nje ya nchi  kufuatia kulegezwa  kwa mashari ya usafiri wa kimataifa kama ilivyoagizwa na rais Uhuru Kenyatta .

Ndege ya kwanza ya KQ kufnya safari ya kimataifa  KQ100  imeondoka mapema leo kwenda lOndon ,Uingereza

Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo Michale Joseph  amesema ziara hiyo ya kwanza ni muhimu sana na yenye hisa nyingi  akisema kwamba hali imekuwa ngumu kwa wafanyikazi wa kampuni hiyo .

Joseph ni miongoni mwa walio katika ndege hiyo kwa safari ya kwenda London .

KQ 2

KQ 3

Mwezi huu kutakuwa na  ongezeko la safari za kimataifa kwenda katika miji ya Paris , Mumbai na Amsterdam .

Barani Afrika KQ itafanya safari za kwenda  Accra, Dzaoudzi, Freetown, Harare, Kilimanjaro, Lagos, Monrovia, Moroni, Nampula  na Zanzibar.  Kulingana na uhitaji ,safari  zaidi zitafanywa katika maeneo mengine  duniani .

Katibu wa utawala wa mashauri ya Kigeni Ababu Namwamba amesema ni jambo zuri kushuhudia hatua za kuanza kufunguliwa kwa uchumi .

 

Shirika hilo linata sanitizer kwa wasafiri wote walio katika ndege hiyo  na wafanyikazi wake .

Janga la covid 19 limekuwa na athari kubwa kwa sekta za usafiri  wa ndege na utaii baada ya mataifa mengi kupiga marufuku safari za kimataifa .

Kulingana na IATA  mapato yatonakayo na usafiri wa ndege yamepungua kwa dola bilioni 6 ikilinganishwa na mwka jana .

Sekta ya utalii nchini Kenya nayo imepoteza  shilingi bilioni 80  kufikia sasa .

 KQ 4

KQ 5

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments