PICHA: Kutana na babake mwanamitindo Vera Sidika

Mwanamtindo Vera Sidika kwa mara ya kwanza amewaacha mashabiki wake na butwaa baada ya kuchapisha picha yake na babake mtandaoni.

Vera alichapisha picha hiyo akiwa amebebwa na babake akiwa mdogo.

Isitoshe, mwanamtindo huyo ambaye kwa sasa wanachumbiana na mtanzania Jimmy Chansa baada ya kuachana na mwanamziki Otile Brown, alieka cheti chake cha kuzaliwa kwenye mtandao akitaka kuthibitisha kuwa jina lake sio "Veronica" kama iliyvo ada ya watu wengi kumuita hivyo, bali anaitwa "Vera", huku akiongeza kuwa alizaliwa hospitalini Agha Khan.
Vera pia alimuonesha mamake mzazi mtandaoni, mwaka jana, huku pia akithibitisha kuwa ana miaka 28 na sio 21. Mwanamitindo huyo kwa sasa ni afisa mtendaji mkuu katika kampuni ya veetox tea na pia Vera sidika beauty parlour.