Picha kutoka familia ya Massawe Japanni zitakupa hamu ya Krismasi!

Imesalia masaa machache sasa kabla dunia nzima isherehekee kuzaliwa kwa mwokozi yesu kristo, dunia nzima. Hata hivyo, hilo halijamzuia kipenzi chetu cha redio, Massawe Japanni na familia yake kuanza sherehe mapema.

Massawe, mumewe Tom Japanni na wanao, wasichana watatu warembo walikusanyika kwao nyumbani na kupiga picha murua kabisa wakiwa na nguo zao za Krismasi.

Picha hizi ambazo zimepigwa na mwanahabari wetu, Victor Imboto zinaonesha furaha tele, upendo na mapenzi yaliko katika familia hii ya Japanni.

Kingine kinachofurahisha macho ni jinsi Massawe Japanni alivyorembesha nyumba yao kwa kununua mti wa krismasi na kuurembesha na zawadi na mapambo ya krismasi.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Massawe alichukua fursa hii kuwatakia mashabiki wake na wakenya krisimasi iliyojawa na furaha na upendo.

Aliandika,

Merry Christmas from us!!!!

Katika ujumbe mwingine tofauti aliandika,

Season to be jolly!!!

Kutoka kwa familia ya Massawe na familia kuu ya Radio jambo tunawatakia nyote krismasi iliyo na fanaka na baraka zake mwenyezi mungu!