EIso5rNXUAAP2Nn

(+ Picha) Levis Saoli atua Citizen TV, alichokisema Nimrod Taabu,Joe Ageyo

Ndoto ya muda mrefu ya Levis Saoli kuonana na Nimrod Taabu imetimia.

Hii ni baada ya kijana huyu kupata mwaliko katika runinga hii.

Levis Saoli ambaye ana umri wa miaka 15 alipata sifa kedekede katika mitandao ya kijamii baada ya kuripotia runinga ya Citizen taarifa iliyogusia swala la msitu wa Mau

Hatutaki vituo vya polisi Kibra, MacDonald Mariga

Kijana huyu wa shule ya upili alionyesha talanta na ubunifu alionao.

Kipaza sauti alichoshika kilikuwa na nembo ya kujitengeneza ya Citizen TV.

Katika kipindi cha Sema Na Citizen, Nimrod alimhimiza kijana huyu azidi kujituma.

EIso5rNXUAAP2Nn

“Video nyingi zaidi endelea tu kuporomosha na tutakuwa tunasaidiana na wewe kuweza kukushika mkono”

Aidha, alimuomba asome taarifa ya habari na kwa ujasiri Levis akaisoma,

“Mtazamaji tunaendelea na taarifa zetu. Serikali imeweka mikakati ili kuhakikisha mitihani ya KCSE haiibiwi…” Aliendela Levis.

Mkurugenzi Joe Ageyo amefunguka katika mtandao wa Twitter na kusema kuwa kijana huyu ana nafasi kubwa zaidi,

“Levis Saoli atavuka mipaka na kwenda mbali zaidi. Ni mwerevu, ana ml_ahaka mwema na hekima kuhusu habari na matukio yanayoibuka…” Alichapisha Joe Ageyo.

(+ Picha) Levis Saoli atua Citizen TV, alichokisema Nimrod Taabu,Joe Ageyo(+ Video) Rosa Ree aomba wafuasi wake radhi, video chafu na Timmy

Alifunguka zaidi kuwa kijana huyu wa shule ya upili atapata mafunzo kutoka kwa wasomaji habari na kuwa kituo hiki kitamkuza ili kufikia kilele cha ndoto zake.

“Kwa kweli tumevutiwa na kipaji chake na tunataka kuona uwezo wake. Tunampa mafunzo kwa sasa na anaruhusiwa kuingia studio zetu na kutangamana na wasomaji habari wetu…” Alisema Ageyo.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments