Picha: Misa ya wanafunzi walioaga yafanyika Kakamega

WhatsApp.Image.2020.02.07.at.5.44.56.AM
WhatsApp.Image.2020.02.07.at.5.44.56.AM
Madhehebu tofauti yaliandaa maombi hii leo huko Kakamega kwa ajili ya wanafunzi 13 kati ya 14 waliofariki kufuatia mkanyagano kwenye shule ya msingi ya Kakamega, jumatatu.

Matokeo ya uchunguzi wa maiti yalifichua jana kuwa watoto hao walifariki kutokana na kukosa hewa ya kupumua.

Katibu mkuu wa chama cha waalimu KNUT Wilson Sossion ameisuta wizara ya elimu kwa utepetevu wake uliosababisha kifo cha wanafunzi hao 14. Sossion anasema mkanyagano huo ulitokana na msongamano wa wanafunzi hao kitu anachosema kingeshughulikiwa mapema kwa kutekeleza ripoti ya ubora wa ujenzi.

Tazama picha hii;