Afisa mkuu mtendaji wa Hospitali ya Kijabe Ken Muma amesema hawawezi kufichua lolote kwa sababu ya familia na jukumu la hospitali kulinda usiri wa wagonjwa .Tuju alikimbizw akatika hospitali ya AIC Kijabe pamoja na mlinzi wake na dereva na wasamaria wema baada ya ajali hiyo iliyohusisha matatu walipokuwa wakienda Kabarnet ,Nakuru kwa maazishi ya Marehemu Mzee Daniel Moi .
Tazama video ya Tuju akiingizw akatika hospitali ya Karen .
https://twitter.com/YusufJumaKenya/status/1227594300768358400
Gari la Tuju liligongana na matatu yachama cha ushirika cha Nuclear Sacco, iliyokuwa ikija Nairobi . Gavana wa Machakos Alfred Mutua ,waziri wa Spoti Amina Mohamed,waziri wa ICT Joe Mucheru na waziri wa Uchukuzi James Macharia walimtembelea Tuju hospitalini .