(+ Picha) Paul Manyasi aliyeanguka kutoka kwa ndege anga za London

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ kiliwatia wengi hofu kubwa.

Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa KAA.

Aidha, mamlaka ya ndege nchini imekana taarifa kuwa Paul alikuwa mfanyakazi wao.

Mwili wa kijana huyu ulianguka kwa kishindo huku shimo kubwa likichimbika katika shamba la maua kusini mwa mji wa London.

Kisa hiki kilifanyika Juni 30 mwaka huu.

Baadaye picha za kijana huyu zilipatikana na wazazi wake kutambuliwa.

Aidha, shirika la habari la Sky News limebaini kuwa jamaa huyu alitoka Magharibi mwa Kenya.

Tazama picha za kijana huyu