PICHA: Tazama jinsi Massawe Japanni alivyosherehekea siku ya kuzaliwa

Jumamosi iliyopita, mrembo wetu Massawe Japanni aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Mtangazaji huyo wa Bustani la Massawe, alipepea hadi Mombasa pamoja na marafiki zake wa karibu ambapo walijibamba kupindukia ndani na pia nje ya bahari.

Akiwa huko, Massawe alipata fursa ya kukata keki pamoja na wapendwa wake huku akiendelea kuburudika katika likizo yake ndogo.

Massawe alichapisha ujumbe murwa katika mtandao wake wa Instagram huku akitupa nafasi ya kutazama jinsi mambo yalivyokuwa huko pwani.

Aliandika,

In the end, it’s not the years in your life that count, it’s the life in your years. God has been faithful to me!

Mpiga picha wetu, Victor Imboto naye alikuwa mle kupiga picha za kishua.

Tazama picha zifuatazo.