Watoto hawa wanne wanazidi mastaa hapa nchini kwa mashabiki Insta.
Tiffah ana wafuasi 2,300,000
Prince Nillan anafuatwa na watu 919,000
Daylan mtoto wa Hamisa Mobeto ana wafuasi 457,000
Naseeb Junior anafuatwa na watu 105,000
Aliitwa jina hili kwa sababu alizaliwa siku sawa na ya babake.
Staa huyu wa mkwaju wa Baba Lao alikata keki na wauguzi katika hospitali ya Agha Khan punde tu Naseeb Jnr alizaliwa.
Baada ya siku 40 , wazazi wa Naseeb Jnr waliita marafiki katika nyumba ya Diamond iliyopo On Tuesday the Dar es Salaam, Tanzania ili kusherehekea.
Katika mila na desturi za waislamu, mtoto na mamake wanatakiwa wakae ndani hadi siku 40 ili mwanamke apate muda wa kupumzika.
Mastaa Tanzania walifika katika hafla hiyo wakiwemo Rayvanny, Lava Lava, Mbosso, Mama Dangote, Queen Darleen, Esma Khan na Wolper miongoni mwa wengine.
Aidha, familia ya Tanasha haikufika katika sherehe hizo.