Picha ya mama Diamond na mumewe yazua cheche za maneno

78752470_566482030564984_9164910187562139648_n
78752470_566482030564984_9164910187562139648_n
Mapenzi mazito kati ya mama Diamond na mumewe Shamte yamezidi kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Msimu huu wa krismasi, Shamte ameonyesha mapenzi ya kweli katika sehemu ya kuogelea.

Picha hii ya wapenzi hawa wawili imezua cheche za maneno huku baadhi ya wafuasi wake wakisema sio poa.

"Duh, Mungu wangu! Hii sasa ni shida mpaka naona aibu licha ya kwamba picha imepigwa na mtu mwingine, lakini aibu naiona mimi..."

"Inakuwaje mama mwenye mtoto mkubwa kama Diamond, tena staa kufanya hivi, mwanaye sijui huwa anajisikiaje,” alilalamika mfuasi wa mama huyu Insta.

https://www.instagram.com/p/B5-Qfxih4q8/

Haya yanajiri huku mumewe akinukuliwa kusema kuwa hajamuoa mama huyu kwa tamaa ya hela.

"Kwa jinsi unamwona huyu bibiye wewe, ushawahi kumskia akaonga mtu?Hakuna mtu anapata hela kwake yeye. Bibi huyu alikuwa rafiki yangu,urafiki ukatengeneza mahusiano, mahusiano yakatengeneza mke na mume...' alisema Shamte.