Picha ya siku: Dereva wa taxi avalia 'mask' akiwa amebeba wachina

Dereka wa taxi ambaye alikuwa amebeba wateja wachina kutoka uwanja wa ndege wa JKIA alionekana akiwa amevalia mask usoni katibu na chuo kikuu cha Daystar.

Picha hii imesambaa mitandaoni kama moto jangwani.

Hili lawadia punde tu baada ya wizara ya afya kuchunguza visa au tahadhari 17 vya virusi vya COVID-19 ila hakuna kisa kilichoripotiwa.

Jumanne, Februari 25, tahadhari mbili za virusi hivyo zilitolewa, moha katika barabara ya Riara na nyingine Valley Arcade kabla ya kuchunguzwa.

Kulingana na shirika la afya duniani, WHO, ni visa 80239 vya Corona Virus vilivyoripotiwa huku watu 2700 wakipoteza maisha yao.