Safari ya mwisho;picha za mwisho za mazishi ya hayati Mzee Daniel Arap Moi

Aliyekuwa rais mstaafu wa Kenya hayati Daniel Arap Moi aliaga dunia mapema mwezi wa Februari mwaka huu, Moi aliekwa katika jumba la bunge ili wananchi waende kuona mwili wake kwa siku tatu.

Moi alisifiwa kwa mengi huku viongozi wengi wakisimulia vile walikosana na Moi na kisha wakasamehana.

Moi alizikwa jana nyumbani kwake Kabarak kaunti ya  Nakuru, huku ibaada ya wafu  ikifanyika katika shule ya Kabarak na mwisho kusafirishwa nyumbani kwake kuzikwa katika mazishi ya kipekee na ya kibinafsi.

Askari wa jeshi walifyatua risasi kumi na tisa hewani ili kuonyesha heshima yake ya mwisho.

Ni jambo au kisa kilichotangazwa katika redio,runinga na hata kwenye magazetti.

Katika kumbukumbu za mzee Moi maziwa ya nyayo ndio iliweza kua kipa umbele katika kumbukumbu zote.

Hizi hapa baadhi ya picha za mwisho za mazishi hayo;