(+ Picha)Mume wangu hakuwahi kupigana kuni kabla anioe, Susan Munene

Screenshot_from_2019_12_17_10_28_59__1576567774_20292
Screenshot_from_2019_12_17_10_28_59__1576567774_20292
Muhubiri aliyevuma na tamko la Twa Twa Twa amefunguka kuwa mumewe alimuoa akiwa bado bikra.

Susan alichangamsha mitandao ya kijamii katika video aliyosikika akitoa sauti ya Twa Twa akiashiria tendo la ndoa.

Wengi walimsifia kwa kusema bila kuficha kitu na ambacho wengi huhofia kusema..

Susan aidha amewataka vijana kudhibiti hamu zao za kufanya mapenzi ili kujiepusha na mimba za mapema.

"Kati ya vitu na ambavyo napenda sana kutoka kwa mume wangu ni kuwa alinioa akiwa bikra kabisa..."

Mumewe alimuunga mkono zaidi wakati kipande hicho cha video kilisambaa.

"Ahsante mke wangu kwa kuruhusu mungu akutumie kuponya ndoa nyingi. Una baraka zangu na nakuunga mkono," Munene.