Katika shule ya msingi ya Kihumbuini , Kangemi, mwalimu mkuu Hassan Tala aliwaongoza walimu wake kurejea shuleni huku akiketi mbali na kila mmoja kutii kanuni za kupambana na covid 19 .
Mwalimu mwingine alikuwa darasani akifuta ubao na kuyapanga madawati ya wanafunzi ili kuweka umbali wa dawati moja hadi la pili .
Katika shule ya Moi Avenue Primary walimu na wazazi walifanya ukaguzi wa vyoo .walimu baadaye walifanya mkutano kupanga ratiba yao pindi shule zitakapofunguliwa .
Wiki jana baraza la magavana lilitangaza kwamba shule za chekechea zitafunguliwa mwezi mmoja baada ya shule nyingine kufunguliwa ili kukadiria matayarisho .
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihutubia taifa baadaye jumatatu baada ya kuandaliwa kwa kongamano linalofanywa kwa njia ya mtandao kuhusu Covid 19 na ataratibu mikakati ya kufunua nchi na sekta za uchumi na jinsi hali itakavyokuwa sasa baada ya janga la Covid 19