Pigo kwa Magufuli! Bunge lasitisha vikao vyake baada ya mbunge mwingine kufariki

Tanzania-Parliament-730x414
Tanzania-Parliament-730x414
NA NICKSON TOSI

Bunge la Tanzania limelazimika kusitisha vikao baada ya mbunge wa Sumve Richard Ndassa kufariki akiwa Dodoma.

Ndassa wa miaka 61, alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi tangazo lilothibitishawa na spika wa bunge hilo Job Ndugai japo hakuelezea kilichosabibisha kifo chake.

Rais Magufuli alituma risala zake kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mbunge huyo na kumtaja kama mtu shupavu aliyetekeleza kazi yake vyema.

“I recall in 1995 when Ndassa and I became members of Parliament. He was an MP for Sumve constituency and I was the MP for Biharamulo East which is now known as  Chato constituency. May his soul rest,”  alisema Magufuli

Yanajiri hayo huku taifa hilo pia likiomboleza kifo cha waziri wa katiba na haki bwana Mahiga ambaye alifariki akiwa na miaka 72.

Kwa sasa, Tanzania iko na visa 480 vya Maambukizi ya virusi vya Corona.