Ruto amesema alitaka Jubilee kuwa na mgombeaji katika uchaguzi huo na siku ya jumatano alionyesha masikitiko wkamba Jubilee imeamua kumuunga mkono mgombeaji wa ODM.
Siku ya alhamuisi Ruto alikutana na gombeaji huru Feisal Abdallah Bader anayetaka kuichukua nafasi hiyo baada ya kifo cha Suleiman Dori .
Kupitia Twitter Ruto alisema amekutana na mgombeaji huyo aliyeandamana na wabunge wengine wa pwani .
Waliokuwa katika mkutano huo ni wabunge
Athman Shariff (Lamu East), Mohammed Ali (Nyali), Owen Baya (Kilifi North), Khatib Mwashetani (Lunga Lunga) na Aisha Jumwa (Malindi)
Sharlet Mariam, aliyekihama cha ODM alisababisha kizaazaa katika makao makuu ya Jubilee akitaka kupewa tiketi ya chama hicho kugombea uchaguzi huo mdogo .
Ruto alimtambua Mariam na kusema iwapo ataitisha usaidizi wake kuwania kiti hicho kama mgombea huru basi atakuwa tayari kumpiga jeki .
Seneta wa Nairobi Johnstone Sakaja amesema sio kwa maslahi ya Jubilee kutokuwa na mgombeaji katika uchaguzi huo mdogo .
Kwa sababu chama hakina mgombeaji basi wanachama wana uhuru wa kumuunga mkono wanayemtaka .Rais hatomfanyia kampeini mgombeaji yeyote’ amesema Sakaja .