• Kwenye Songa Play, utajiburudisha na podkasti kama Patanisho ya Gidi na Ghost, Toboa Siri ya Mbussi na Lion, DeadBeat ya Massawe Japanni na ladha ainati za muziki unaokufurahisha.
Shirika la habari la Radio Africa limeboresha hata zaidi jinsi mashabiki wa chapa zake mbalimbali wanaweza kufuatilia vipindi vyao pendwa kupitia jukwaa jipya la Songa Play.
Jukwaa la Songa Play, lilizinduliwa takribani wiki tatu zilizopita na tayari limepata ufanisi mkubwa na mapokezi ya kishujaa kutoka kwa mashabiki wa chapa za Radio Africa.
Songa Play ni jukwaa ambalo ni kama ghala lenye vipindi vyote vya stesheni zote za shirika la habari la Radio Africa, na kipengele cha kufurahisha zaidi ni kwamba mtu hahitaji kulipa hata senti ili kujipakulia burudani alipendalo.
Katika jukwaa hili, si tu miziki utapata, bali pia unapata vipindi vyote vya stesheni za Radio Africa, wakati wowote unahitaji, ni wewe tu na simu yako!
Stesheni zote, zikiwemo Radio Jambo, Kiss 100 FM, Classic 105, Gukena FM, Home Boyz na East FM zina vipindi vyao vyote katika jukwaa la Songa Play ambavyo vinapeperushwa kwa saa 24 kila siku ya wiki.
Vipindi hivyo ni pamoja na podkasti pendwa zinazoifanya stesheni ya Radio Jambo kupepea na kutawala mawimbi ya utangazaji Kenya kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Kwenye Songa Play, utajiburudisha na podkasti kama Patanisho ya Gidi na Ghost, Toboa Siri ya Mbussi na Lion, DeadBeat ya Massawe Japanni na ladha ainati za muziki unaokufurahisha.
Je, ni vipi unaweza kupata burudani hili la bila malipo?
Ni rahisi, ingia kwenye simu yako, tafuta tovuti ya www.songaplay.com ama pakua program kwenye Google Play Store ili uwe katika ukurasa sawa na maelfu ya Wakenya wanaoburudika kwa hisani ya Songa Play.