Pogba agombana na Lingard siku ya kwanza

Kiungo wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba alijipata kwenye majibizano na kiungo mshambulizi Muingereza Jesse  Lingard siku yao ya kwanza, baada ya kurejea mazoezini kutoka likizoni.

Baada ya kuamrishwa kurejea kwenye maandalizi ya msimu mpya, Paul Pogba alionekana kukataa amri za wakubwa wake huku kukiwa na uvumi kwamba huenda mkali huyo wa Ufaransa akaigura Manchester United na kujiunga na Real Madrid ya Uhispania.

Hata hivyo, Pogba alirejea kwenye kambi ya mazoezi siku ya jumatatu na jambo la kwanza lilikuwa ni kugombana naye Lingard, huku wawili hao wakitenganishwa na Victor Lindelof.

Kwingineko ni kwamba babaye Neymar amesema kuwa mshambulizi huyo wa Brazil atarejea mazoezini tarehe 15 baada ya kukosa kufika siku ya kwanza. Rais wa PSG, Leornado alisema kuwa iwapo kuna klabu itatoa hela yake Neymar basi wao wapo tayari kumuachilia.

Mshambulizi wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann huenda akaadhibiwa na klabu hio ya Uhispania kwa kukataa kuwasili mazoezini kama ilivyo tarajiwa siku ya jumatatu. Griezmann anayetarajiwa kujiunga na klabu ya Barcelona, yumo mbio kutoka uwanjani Wanda Metropolitano.

Klabu ya Leicester imekamilisha uhamisho wa kiungo wa ubelgiji na AS MOnaco ya ufaransa Youri Tielmans kwa ada ya pauni millioni 40. Mbelgiji huyu ametia sahihi mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa msimu wa 2015/2016 liguu nchini uingereza.

Klabu ya liverpool ipo tayari kumpa mshambulizi mkenya, Divock Origi mkataba wa muda mrefu. Origi alirejea kutoka likizoni jumatatu na msemaji mkuu wa Liverpool ameeleza kuwa mabingwa hao wapo tayari kumpa Origi shukrani kwa njia ya kipekee kwa kumuongezea mkataba mwingine.

Hatimaye ni kuwa mshambulizi wa klabu ya West Ham Marko Anautovic amekamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya China Shanghai SIPG kwa dau la millioni 22.5. Mshambulizi huyu anajiunga na aliyekuwa kiungo wa Chelsea mbrazili Oscar.