Mkurugenzi wa Mashtaka Noordin Haji/ Maktaba

Polisi 2 walioshutumiwa kwa mauaji ya raia wawili wa Garissa kusalia korokoroni

Maafisa wawili wa upelelezi walioshtakiwa kwa mauaji ya raia wawili katika kaunti ya Garissa watasalia korokoroni wakisubiri kuamuliwa kwa ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana.

Hii ni baada ya mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji kupinga kuachiliwa kwa wawili hao Adan Salat  na Abdirahman Samow kwa dhamana, akitaja usalama wao na uwezekano wao kuhitilafiana na mashahidi.

Adan na Abdirahman walifika mbele ya jaji wa mahakama kuu Jessie Lessit. Katika ombi lake DPP alitaka washukiwa kunyimwa dhamana kwa msingi kwamba wanakabiliwa na shtaka kubwa la mauaji ambalo lina kifungo cha kunyongwa ikiwa watapatikana na hatia.

Court-Gavel-Thumb
Court-Gavel-Thumb

Wawili hao walikanusha mashtaka dhidi yao. Walishtakiwa kwamba mnamo Julai 25 katika eneo la Soko Ng’ombe walishirikiana kuwaua Aden Abdi Madhobe na Mudhidin Aden Mudhow.

Upande wa mshtaka ulisema kwamba ikiwa wawili hao wataachiliwa kwa dhamana huenda wakavuruga mashahidi wakuu ambao ni wananchi wa jamii ya Garissa Township.

Photo Credits: Maktaba

Read More:

Comments

comments