Afisa mmoja wa polisi amezira na kisga kuaga dunia siku ya jumatano baada ya kumzaba jamaa mmoja kofi aliyekuwa amejumuika nawe kula miraa katika kaunti ya kakamega
Polisi huyo Remko Madowo alikuwa ameketi katika eneo la kula Miraa kwenye kituo cha kibiashara cha Malava wakati mwanamme mmoja ambaye hakutambuliwa alipojiunga naye .
Kulingana na ripoti ya polisi katika kituo cha Kabras Madowo alimuuliza jamaa huyo mbona alikuwa ameketi hapo naye na kumzaba makofi mawili . Bila kusema jambo mwanamme huyo aliamka na kuondoka huku akiapa kuripoti tukio hilo katika kituo cha polisi .
Polisi huyo wakati huo huo alianguka na alipokimbizwa hospitalini ,madaktari walisema alikuwa ameaga dunia .
Madowo alikuwa amehamishwa kutoka kituo cha polisi cha Kabrqas hadi katika kituo cha Kongit huko Bungoma .Alikuwa amerejea Kabras kuchukua vitu vyake