Polisi bandia wapotea na milioni 72 kutoka ATM ya Standard Chartered na gari ya G4S Nairobi

unnamed__1___1567686417_28749
unnamed__1___1567686417_28749
Wanaume waliokuwa wanaigiza kama maafisa wa polisi leo asubuhi wameripotiwa kuiba mifuko 13 iliyojaa kitita cha mamilioni ya pesa kutoka benki ya Standard Chartered na G4S hapa jiji kuu la Nairobi.

Maafisa wa polisi wametoa taarifa kuwa washukiwa hao waliiba kitita hiki cha pesa kutoka kwa gari ya kusafirisha ya G4S na baadaye kuvamia benki na kufagia kiasi kikubwa cha pesa.  Thamani ya pesa zilizoibiwa ni Milioni 72 iliyojaa katika magunia 13.

Soma hadithi nyingine hapa:

“Walipofika waliomba kupewa neno siri waliyotumia kufungua mashine ya ATM." Shajara ya polisi ilionyesha katika kituo cha polisi Lang'ata.

Wilfred Nyambane ambaye ni afisa anayesimamia idara ya usafirishaji hela katika shirika la G4S amethibitisha wizi huo.

“Maafisa waliojifanya kuwa wanawekea ulinzi hela walibadilika ghafla na kuwa majambazi sugu na kuwalazimisha kuchukua simu zao za rununu. Hapo ndio walitoa pesa zote na kuzipakia katika gari aina ya Toyota Noah na wakatoroka na takriban milioni 72." Maafisa wa polisi wamesimulia.

Soma hadithi nyingine hapa:

Wafanyakazi wa kampuni ya wameeleza kuwa wezi hao walisema wanataka pesa iliyokuwa inasafirishwa na neno siri za mashine za ATM za benki yaStandard Chartered. Tukio hii iliripotiwa mwendo wa saa mbili asubuhi.

Sasa maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi wa kina kuwasaka wahalifu hao.