Polisi Bungoma Wamsaka Mshukiwa Wa Ubakaji Wa Mwanafunzi Wa Shule Ya Moi

Huku hisia mseto zikizidi kutolewa kutoka kwa wakenya kote nchini kuhusiana na ubakaji dhidi ya wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Moi jijini Nairobi, polisi wa Kimilili kaunti ya Bungoma wanamsaka mwalimu mmoja wa shule ya upili ya wasichana ya Moi Kamusinga ambaye ameenda mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa miaka kumi na nne wa kidato cha pili mnamo siku ya jumapili iliyopita.

Naibu kamishina wa Kimilili, Reuben Loyotoman amesema mshukiwa kwa Jina Willy Masikari Wanyonyi na ambaye ameajiriwa na bodi ya shule hiyo, huenda amekuwa na hulka hiyo kisiri na mwanafunzi huyo.

OCPD wa Kimilili Gladys Rutera amethibitisha kisa hicho na kusema kwamba polisi wanafanya kila waewzalo kumtia mbaroni mshukiwa huyo.

Brina Ojamaa