Polisi Bungoma Wasaka Majambazi Waliotekeleza Mauaji Ya Watu Watano Wakiwemo Watoto

bungoma
bungoma
Maafisa wa polisi Bungoma bado wanawasaka watu waliotekeleza mauaji ya watu watano wakiwemo watoto na kuwabaka watu wakike watatu usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Masaek eneo la Kutere eneo bunge la mlima Elgon.

Wakaazi wa kijiji hicho wakiongozawa na Mary Chemutai ambaye bwanake alipigwa risasi wamesema watu hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki na vifaa vyenye makali waliwavamia wakaazi hao usiku saa sita za usiku.

Majambazi wawili waliuawa kwa kupigwa na wakaazi waliokuwa na hamaki katika kijiji cha kapsambu eneo hilo la mlima elgon.

-Brian Ojamaa