Polisi kumpiga mke wake risasi baada ya mgogoro wa kifamilia

unnamed(5)
unnamed(5)
Afisa wa polisi wa Utawala alimpiga mke wake risasi. Hii ni baada ya kuwa na mgogoro wa kifamilia eneo la Navakholo kaunti ya Kakamega.

Kisa hicho kilitokea Alhamisi usiku, inamaana polisi huyo hajui kutumia silaha yake ipasavyo?

Polisi huyo aliweza kutoweka baada ya kumuuwa mke wake ambaye ni mwalimu katika shule ya upili ya Navakholo, wakazi waliweza kuandamana baadaye na kuwazuia polisi kuchukua mwili wa marehemu.

Walisema kwanza matakwa yao yaweze kutimizwa kwa polisi kumleta muuaji huyo kwanza ili waweze kubali mwili wa marehemu kuchukuliwa.

Iliwabidi polisi waweze kuwatawanya wakazi hao ili waweze kuchukua mwili huo, hali jawekwa wazi kwanini wapenzi hao waliweza kuwa na mgogoro uliosababisha kifo hicho.

CID wa kaunti ya Kakamega John Onyango alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa polisi huyo hajaweza kukamatwa.

"Hatujui polisi huyo aliweza kupiga risasi ngapi, lakini polisi wako katika tukio la kisa hicho." Alisema John.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kakamega.

KWINGINEKO: Nikuwa...

Watu watatu wamefariki kufuatiana mapigano mapya kati ya Borana na Gabra katika eneo la Haro Giresa kata ndogo ya Saku.

Wengine walipata majeraha ya risasi baada ya mapigani Jumatano, waliweza kupelekwa katika hospitali ya Marsabit kwa matibabu, polisi wa usalamu wametumwa katika maeneo hayo ili kutuliza jambo hilo.

OCPD wa eneo hilo la Marsabit Benjamin Mwanthi alithibitisha kisa hicho na kuwaambia wananchi waweze kutulia kwa sababu polisi wanashughulikia kisa hicho.

Mwenyekiti wa baraza la madhehebu Mohamednur Kuli aliwaambia wakazi kuwa waweze kuwa na amani kwa sababu umoja na amani ndio unaweza kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Mvutano kati ya jamii hizo mbili umekuwa kwa muda mrefu na ambao umeweza kufanya watu wengi kufariki hapo awali.