Polisi kumtafuta mwanaharakati wa Dandora aliyepotea

Kumtafuta kwa wenzake Caroline Mwatha kuliambulia patupu siku ya Alhamisi.

Waliweza kumtafuta kupitia simu yake ilhali ilikuwa imezimwa.

Rafiki yake Mwatha alidai kuwa aliweza kumpigia simu Jumatano 6 jioni lakini hakuweza kupokea simu yake. Kituo hicho kiliweza kumtuma mfanyakazi mwenzake ili aende kumuangalia kwake.

Alipata msichana wake Caroline aliye na miaka 13 akiwa peke yake nyumbani mwake, kupotea kwa mwanaharati huyo kuliweza kuripotiwa katika kituo cha polisi cha Buru Buru.

Jana baba yake Caroline, Stanislas Mbai, alisema kuwa walimtafuta katika hospitali ya Kenyatta, Mama Lucy, hospitali ya Dandora na pia katika chumba cha kuifadhi maiti cha mji.

"Tunafanya lolote tuwezalo, na tunaamini kuwa yuko uhai kwa maana mvulana wangu na rafiki zake walienda kumtafuta kila nyumba yoyote ya kuifadhi maiti na hawakuweza kumpata," Alieleza Mbai.

Polisi katika kituo cha Buru Buru waliweza kuchukua kauli kutoka kwa majirani wake na pia wazazi wake Caroline. Wazazi wake wanaishi kilomita moja kutoka katika maeneo ya mwanaharakati huyo.

Leo polisi hao wanatarajiwa kuchukua rekodi za simu za Caroline.

Caroline ambaye ni mama wa watoto wawili, mvulana ambaye yuko shule ya kulala ya mji na msichana ambaye kwa sasa anaishi na mababu wake.

Mume wa mwanaharakati huyo anafanya kazi katika nchi ya Dubai na ambaye anatarajiwa kufika nchini hivi leo.

Jana wanachama wa Lobby waliweza kupatwa na wasiwasi waliposikia kuwa kuna mwili ambao umepatikana katika mto wa Nairobi, walienda kuangalia kama ulikuwa wa Caroline lakini waliweza kupata kuwa mwili huo ulikuwa wa mwanaume.

Amnesty International iliweza kuwaomba polisi kumtafuta mwanaharakati huyo na kupotea kwake haraka iwezekanavyo.

"Amnesty International Kenya linawaita Kurugenzi ya uchunguzi wa makosa ya jinai na huduma ya polisi ya kitaifa kuchunguza kilicho mfanya Caroline apotee, na kuwajulisha marafiki na familia hali yake na aliko, Irungu alisema katika kauli.

Mratibu wa kituo hicho Wilfred Olal alisema kuwa wanaharakati ama watetezi wa haki hawana uhusiano mzuri a polisi.

"Unapokuwa unahusika na kesi ya mauaji ya polisi, unawamulika maafisa wa polisi maalum ambao si wazuri kwetu,"Alisema kwa simu.

"Polisi muuaji amekuwa adui sana na kutoa vitisho kati ya wenzetu ikiwemo Caroline ambaye hatujui alikoenda,"

Mwaka jana Oktoba waliweza kueka kumbukumbu ya mauaji baridi, ya watu sita na polisi kulaumiwa kwa mauaji hayo, katika eneo la Gitwamba Dandora, phase V Kinyango.

Bosi wa Buru Buru Geoffrey Mayek aliweza kuwaambia wanahabari sita hao walipigwa marisasi na kufariki baada ya kuiba pikipiki na kubaka abiria wa eneo hilo, mashahidi walipinga.

Kupitia kituo cha haki cha Dandora mashahidi waliweza kusema vile polisi waliwakimbiza wezi hao waliokuwa wameripotiwa kumbaka mwanamke mmoja kisha kuiba pikipiki.