Polisi Mwatate wanamzuilia jamaa aliyemkata Mjomba wake Kichwa

Polisi kaunti ya Taita Taveta eneo la Mwatate wanaendelea kumzuilia jamaa wa miaka 20 baada ya kumkata kichwa mjomba wake.

Jamaa huyo inasemekana kuwa alitekeleza unyama huo na kisha kuchukua kichwa hicho na kumkabidhi mkewe mwendazake ambaye alitimuka mbio bada ya kuona ni kichwa cha mumewe.

Mshukiwa huyo alitekeleza unyama huo mnmo Mei 27 mwaka huu katika kitongoji cha Mrughua.

Majirani hata hivyo wamesema kuwa mshukiwa huyo amekuwa akimtishia maisha mjombake siku za hivi karibuni.

Mwili wa mwendazake sasa umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Moi.