Polisi watafuta mwili ya Muhubiri aliyejitia kitanzi huko Matayos

Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wananchi wangali wanausaka mwili wa mwanaume mmoja anayeaminika kuwa muhubiri ambaye alijirusha kighafla kwenye mto sio kwenye daraja linalo unganisha barabara kuu ya busia-kisumu huku akiacha nyuma bibilia na shilingi 40.

Wananachi wanasema kuwa mwanaume huyo alikuwa amebebwa kwa pikipiki kutoka soko la Matayos kuelekea mjini Busia ambapo aliruka kutoka kwa pikipiki hiyo na kukimbia hadi kwa daraja hilo na kujirusha ndani ya maji.

Hatua iliyo mchochea kutekeleza kitendo hicho imesalia kuwa kitendawili.