Polisi Nigeria wabomoa hoteli zalizokiuka sheria za kukaa nyumbani

6f59bfd70de19d7a
6f59bfd70de19d7a
Maafisa wa polisi nchini Nigeria wamebomoa hoteli mbili kwa madai kuwa zilikiuka sheria za kukaa nyumbani. Gavana wa jimbo la Rivers, Nyesom Wike alisema kuwa wamiliki wa hoteli ya Edemete na Prodest walikamatwa kwa kuendesha biashara kinyume na masharti yaliyowekwa kwa ajili ya kukabiliana na COVID- 19.

Nyesom alisema visa vya hivi karibuni vya maambukizi ya COVID-19 vilitokana na watu waliokuwa katika hoteli mbalimbali katika jimbo hilo.

https://twitter.com/Ijay_oma/status/1257667326515781634

Aidha, gavana huyo hakusema iwapo hoteli hizo mbili zilikuwa zimeripoti maambukizi ya virusi vya corona.

Mmoja wa wamiliki wa hoteli hizo alikanusha madai kuwa hoteli yake ilikuwa ikiendesha biashara kinyume na masharti ya COVID-19.

"Hoteli haikua ikifanya kazi na asilimia 70% ya wahudumu walikua wamerudishwa nyumban." Alisema.

Licha ya kujua hatari za virusi vya corona wanakiuka sheria na kufanya mambo yasiyostahili.