Polisi wa gereza kukamtwa baada ya kumuua mpenzi wake

Kwa kweli hawakukosea walipo sema 'love is blind' lakini kwake polisi huyu upendo umekuwa kinyume cha usemi huo, Tairus mwangi ambaye ni polisi katika gereza la Malindi kwa sasa yupo mikononi mwa polisi baada ya kumuua mpenzi wake Purity Karwirwa.

Inaaminika kuwa Tairus alimuua mpenzi wake kwa kumpiga na nyundo mara kadhaa katika sehemu mbalimbali za mwili.

Upasuaji wa mwili wa mwendazake ulionyesha kuwa alipigwa na nyundo mara tano kwa mwili na pia kwa kuteswa alipokuwa akipigwa.

Mifupa ya mikono yake ilikuwa imevunjika huku ikionyesha jinsi alivyokuwa aking'ang'ana kabla ya kukumbana na kifo chake.

Kulingana na marafiki zake Purity uhusiano wao wa kimapenzi ulianza kupitia mtandao wa kijamii wa facebook nhuku wakianza vurugu baada ya muda.

"Kuna siku Tairus alimtumia Purity jumbe za kutisha, aliniambia nanaenda kumshtaki kwa kituo cha polisi ilhali hakuenda." MMoja wao Alisema.

Baada ya vurugu Tairus alimuomba purity msamaha lakini baada ya msamaha polisi huyo alikuwa na vurugu tena, huku ikimlazimu Purity kukimbilia usalama kwa rafiki yake.

"Alinipigia simu na kuniambia kuwa anakuja kulala kwangu kwa maana ana hofia maisha yake." Alisema rafiki yake.

Tairu,26 alimtembelea dadake katika eneo la Muthacha kaunti ya Kiambu, jumatano baada ya dada yake kuenda kutafuta riziki Jumatano alimualika Purity nyumbani hapo ndipo aliweza kufanya kitendo hicho.

Polisi walitembelea eneo la tukio hilo na kupata nyundo aliouwawa nayo Purity, na nguo za polisi huyo na kisha mwili wa Purity.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti, Mwangi alikamatwa akiwa katika eneo la nyamakima alhamisi na atapelekwa mbele ya mahakama ili kushtakiwa kwa mauaji hayo tarehe 13 machi,2020.