Rodgers Ouma, mwenye umri wa miaka 28 pia atahudumia kifungo cha miaka 10 jela kwa kutumia vibaya maamlaka yake na kulipa shilingi laki nne kwa mwathiriwa kama fidia .
Mkurugenzi wa mashtaka ya umma amesema upande wa mashtaka umethibitisha kesi yao dhidi ya mtuhumiwa bila shauku kwamba Ouma alimhadaa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 hadi katika nyumba yake disemba mwaka wa 2019 na kumfanyia unyamahuo .
Haji kupitia kwa taarifa amesema mwanamke huyo alikuwa amekwenda kuripoti kwamba mumewe alikuwa akimlazimisha kutumia tembe za kuavya mimba ilia to euja uzito aliokuwa nao .
Hakimu aliyeshughulikia kesi hiyo Allan Temba amesema Ouma alitumia vibaya maamlaka yake kwa kuahidi mwanamke huyo kwamba angemsaidia na kesi aliokuwa amekwenda kuripoti .