Polisi waanzisha uchunguzi kuhusiana na Kifo cha Mwanahabari Marijan

RADIO-696x464
RADIO-696x464
NA ICKSON TOSI

Maafisa wa usalama sasa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanahabari wa stesheni ya Pamoja Fm Mohamed Hassan Marijan ambaye aliuwawa asubuhi ya leo akitoka kazini karibu na mahakama ya Kibra.

Naibu Kamishna wa Kibra Gideon Ombogi amesema maafisa wa polisi wametumwa kuanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.'

Kifo cha Marijan kilisababisha wananchi kuanzisha uchunguzi wao wa yule aliyetekeleza unyama huo. Mmoja wa washukiwa anayehusishwa na mauaji hayo ametiwa mbaroni huku maafisa wa polisi Kibra wakishutumiwa kwa kulaza damu na wananchi.

Mwili wa Marijan umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City huku uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo chake ukitarajiwa kutolewa na wapasuaji.

Kwingineko ni kuwa katika kaunti ya Kirinyaga, maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha kutatanisha cha mtoto wa miaka 4 msichana  kilichotokea eneo la Gitoo.

Inadaiwa kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa anakunywa bia katika nyumba ya mwanamume mmoja eneo hilo wakati tukio hilo lilipojiri.

Akidhibitisha tukio hilo, mkuu wa polisi Mwea Magharibi Aden Alio amesema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Kangai na Thomas Chomba, mjomba wa mwendazake.