gavel-iStock

Polisi wadai Mwala alikuwa mlevi. Tarehe ya kufikishwa kizimbani yatajwa

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi David Maina ametoa taarifa kuwa muigizaji Mwala atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya uendeshaji mbaya wa gari na kusababisha kifo.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, Mwala alikuwa mlevi akiendesha gari yake na kumgonga Samwel Mwaki na kumuua papo kwa hapo.

Soma hapa:

Vurugu zazuka katika makao ya Knut, Nairobi

Mwala alikuwa akisafiri kutoka Kaloleni kuenda Mazeras mida ya saa tano usiku alipojaribu kupita gari baadaye kutatizika na kugonga Mwaki.

Gari ya Mwala aina ya Toyota Axio alimgonga na kumburuza mita mia moja mwendazake kutoka eneo la ajali. Mwaki alipata majeraha ya kichwani,mikono na miguu baadaye akafariki.

Staa wa nyimbo za injili akiri kushiriki ushoga hadharani. Wengi wapigwa na butwaa

Maafisa wa polisi walitumwa haraka kumsetiri dhidi ya kero ya waendeshaji bodaboda na wakaazi. Mwala aliachiliwa kwa dhamana ya 40,000 pesa taslimu. Mwala anatakiwa kufika kizimbani ijumaa ya wiki ijayo kujibu mashtaka.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments