unnamed

Polisi wafichua A-Z kuhusu kilichosababisha Mwala kuua Samuel Mwaki

Uchunguzi kamili wa maafisa wa polisi unaonyesha kuntu matukio yalivyojiri katika kisa na ambapo Mwala alihusika katika ajali na kupelekea kugonga na kuua Samuel Mwaki.

Mwala ambaye huwa anaigiza kama inspekta mkali wa polisi alijipata katika hali ya utata baada ya kujaribu kupita gari iliyokuwa mbele yake.

Soma hadithi nyingine huku:

Mwanamume asulubiwa Uganda kwa kuunga mkono chama cha NRM

Kwa mujibu wa taarifa za polisi wanaochunguza kisa hiki, gari lake lilitoka barabarani kukwepa kugongana uso kwa uso na gari nyingine na kupelekea kumgonga Samuel.

Mwala alikuwa peke yake katika gari yake ya Toyota Axio. Polisi walimuokoa kutoka kwa hasira za umati uliojawa na ghadhabu.Katika mtandao wa Twitter, Mwala ametuma pole kwa familia ya Samuel Mwaki.

Mchujo wa chama cha ODM sio Agosti 31. Tarehe yasongeshwa mbele

Taarifa zinaonyesha kuwa Mwala alikuwa anasafiri kutoka hafla ya mazishi kuelekea Mombasa alipohusika katika ajali hii. Maafisa wa polisi walifika ghafla kumkinga na wananchi waliotaka kumvuruga baada ya kisa hicho.

Soma hadithi nyingine huku:

ODM yawatema 9 nje ya mchuano wa ubunge Kibera. Nani yuko ndani?

Mwili wa mwendazake ulikimbizwa Coast General Hospital huku gari ya Mwala ikisalia katika kituo cha Polisi cha Rabai huku kesi ikisubiriwa kutajwa kortini.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments