Polisi wakana madai ya kumteka nyara daktari na kumuibia

unnamed (6)
unnamed (6)
Maafisa kumi wa polisi wamefikishwa mahakamani baada ya kushtakiwa kumteka nyara na kumuibia Lucas Monata ambaye ni daktari katika kituo cha afya ya Tassia.

Godhard Mburu, Vincent Maronga, Geoffrey Lotome, Kennedy Atemi, Elijah Odhiambo, Erick Ochieng, Enock Kipkemoi, Alphonse Ochieng, Oscar Opondo, na Paul Mwangi ambao wanahudumu katika idara ya polisi walikataa mashtaka hayo mbele ya hakimu Jane Kamau na waliachiliwa kwa dhamana.

Monata alieleza korti hiyo kuwa kwa hao maafisa kumi, mmoja alitaka kupimwa virusi vya ukimwi huku mwingine akitaka kumwona daktari kwa haraka. Ni katika harakati hizo ambapo maafisa wawili walijitosa ndani ya ofisi ya Daktari Monata na kumuelezea kuwa ameshikwa na anatakikana kufika katika kituo cha polisi ya Pangani.

Maafisa hao walimwambia Monata kuwa yeye ni mhalifu na kuwa walipokea habari alikuwa na gari nyumbani kwake ambalo lina usajili wa Sudan kusini na pia alikuwa na bunduki aina ya AK47. Monata aliwatolea waraka kuthibitisha gari hilo ni lake. Isitoshe maafisa hao walichukua shillingi 261,000 pesa taslimu ya Kenya

Monata alieleza kuwa hakuwa na budi kukubali yeye ni mwizi ili aachiliwe na maafisa hao ambao walimuachilia mwendo wa saa tatu usiku na kumtishia kuwa atauliwa iwapo atataja chochote.

Aidha Monata alipewa nambari ya Mpesa "0707919229" na maafisa hao wakitaka atumie namba hiyo kuwasiliana nao wakati watamhitaji.