Polisi wamsaka mwanamke aliyemnajisi mvulana wa miaka10

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Makueni wanamsaka mwanamke mmoja mwenye umri wa makamo ambaye amedaiwa kumnajisi mvulana wa miaka 10.

Kwa mujibu wa ripoti katika kituo cha polisi cha Kavumbu, mvulana huyo ni mpenzi wa mshukiwa na hata alilala nyumbani kwake usiku huo ambao anasemekana kutekeleza kitendo hicho.

"Mvulana huyo alienda kucheza na mtoto wa mshukiwa wiki iliyopita na akalala nyumbani kwa mwanamke huyo. Mshukiwa alimvua nguo mvulana huyo kisha akampapasa sehemu zake za siri, akamuamuru amnyonye matiti na kisha akashiriki ngono naye." Ilisoma Taarifa ya Polisi.

Mvulana huyo aliambia maafisa wa polisi kuwa alionywa dhidi ya kufichua kilichotendeka kati yake na mwanamke huyo.

Mwathiriwa amefanyiwa vipimo katika hospitali ya rufaa ya Makueni na imethibitishwa kuwa alidhulumiwa kimapenzi. Mshukiwa yuko mafichoni na anasakwa na maafisa wa polisi.

Je, unafikiri wazazi wanawalinda vyema wanao hasa wakati huu ambapo shule zimefungwa kutokana na janga la codid-19?